13 Jul 2026 • Views: 1
Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Bi Fatma Mohamed Khamis amewakata wadau wa wakaguzi wa Ndani wa Taasisi za Serikali Zanzibar,kutoa maoni yao kwa uhuru, kujadili na kupendekeza maboresho yatakayosaidia kupata muongozo bora kwa Taasisi na kuzuia kukabiliana na udanganyifu.
Ameyasema hayo wakati wa ufunguzi wa mkutano wa wadau wa kujadili na kukusanya maoni kuhusu Mwongozo ya Usimamizi wa Vihatarishi vya Udanganyifu katika Taasisi za Umma, katika ukumbi wa Hotel ya Verde Mkoa wa Mjini Magharibi Zanzibar.
Aidha amesema matokeo ya mjadala huo utasaidia kuboresha miongozo na kuifanya iwe nyenzo muhimu katika kuimarisha uwajibikaji, uadilifu na utendaji wa Taasisi za Umma.
Mkutano huo umewashirikisha Wakaguzi wakuu wa Ndani,mMaafisa Mipango,Maafisa Masuuli wa Taasisi za Serikali na Wasimamizi wa vihatarishi (Risk Coordinator).